Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kutoka Chama cha Wananchi (CUF) leo wametoka nje ya ukumbi wa baraza hilo kwa kile wanachodai kuwa ni ukiukwaji wa sheria, ikiwemo kujaza askari Polisi na wengine wakivaa ninja katika uandikishaji wa Daftari la Wapiga Kura unaloendelea visiwani Zanzibar. Wakizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Ofisi za chama hicho Vuga mjini Unguja, wajumbe hao walisema wameamua kutoka kwa lengo la kupinga matukio yanayoendelea…
↧