CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) ni merikebu inayoelea shelabela katika bahari iliyochafuka. Imo safarini, ikipanda na kushuka juu ya mawimbi yenye hasira, ikiwa haijui tena iendako au hata ilikopanga kwenda. Si siri kwamba chombo hicho kimepoteza dira.Tena kina manahodha wengi. Na kama wajuavyo wenye uzoefu wa ubaharia, penye manahodha wengi, chombo huenda kikenda mrama. Inavyoonyesha ni kuwa, kwa kila hali, chombo hicho kinajiendesha kitatanishi. Hata hivyo, yaliyokifika CCM huvifika vyama vya…
↧