NILIPONUKUU maneno aliyoniambia Samwel John Sitta kupitia simu ya mkononi (rudia makala iliyopita), sikujua bwanamkubwa huyu ana kiburi cha kupindukia mpaka. Mshangao niliopata kuhusu hulka yake hiyo baada ya kumsikiliza Septemba 2014, haujapungua uzito. Sikuwahi kumjua kwa sura yake halisi. Na tatizo zaidi linakuja ninapojiuliza hivi mtu huyu mwenye hadhi kubwa kisiasa kutokana na kupata vyeo vikubwa serikalini, anajisikiaje anapoporomosha maneno ya chuki na ubabe? Najisumbua. Mtu na hulka yake…
↧