Mwanasheria na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amefichua kwamba serekali ya Tanzania ilitaka kufichwa juu ya kukamatwa kwa ndege ya Bombardier huko Canada.
Leo kupitia ukurasa wake wa Intagram Lissu amefichua kwamba serekali ilipeleka Waziri wa Mambo ya Nje, Dr. Augustine Mahiga, na Balozi wa Tanzania nchini Canada, Jack Zoka, kwenda Toronto kufanya mazungumzo na kampuni ya Sterling Construction and Engineering Ltd (SCEL) juu ya namna ya kuinasua ndege hiyo.
“Waziri Mahiga na Balozi Zoka waliiomba SCEL isitoe habari za Bombardier kukamatwa hadharani”, ameandika Lissu
Itakumbukwa kwamba kampuni hiyo ya SCFL ndiyo iliyoishitaki Tanzania katika Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi mwaka 2003,baada ya serekali ya wakati huo kuvunja nayo mkataba wa ujezi wa barabara ya Bagamoyo kinyume na taratibu.
Taarifa za hivi karibuni kutoka serekalini zinadai kwamba ndege hiyo tayari imeshaachiwa na iko njiani kutoka Canada kuja Tanzania.