Ilipoishia wiki iliyopita tuliona Abdull akimuaga Fartuun anaondoka na hatorudi tena Somalia, halikuwa jambo rahisi kwa Fartuun kukubali. Fartuun akamuomba Abdull wakutane kwa mara ya mwisho…Endelea…
Ilipofika jioni Fartuun alijikongoja kuelekea alipoelezwa na Abdull kwamba wangekutana, naye Abdull hakutaka kuchelewa kufika katika fukwe na Lido kumuona kwa mara ya mwisho.
“Pole…”, alisema Abdull mara baada ya salamu
“Nitazoeya tu.. wala usijali”, ilikuwa ni kauli iliyotoka katika kinywa cha mwanamke anayeumia moyoni lakini anajikaza kwa maneno yake. Uso wake ulikuwa mtune kidogo, na lips zilizokauka, sauti yake ilikuwa ya chini na kavu.
Abdull aliona jinsi gani Fartuun amesawijika na kuosa raha, alijitahi kadiri ya uwezo wake kuhakikisha anampa maneno ambayo yangemuacha na faraja, lakini likawa ni jambo gumu kidogo.
“Wewe nenda mimi nitakusubiri,hata kama baada ya miaka kumi…”, ni kauli aliyokuwa akiisisitiza Fartuun.
“Inabidi akija mume..uolewe..?
Abdull alimueleza kwamba hakuwa na haja ya kumsubiri kwani asingerudi tena , lakin ilikuwa kama kutia maji pakachani, ni msamiati ambao Fartuun daima hakuuwelewa kabisa. Abdull hakutaka Fartuun amsubiri kwa sababu ya hatari ya tukio wanaloenda kulifanya.
Alimwambia aende lakini atambue kwamba kuna mke amemuacha, na atamkuta kama alivyomuacha wala hangechoka kusubiri hadi atakapo kuja tena. Moyoni mwake aliamini Abdull angaerudi kwa ajili yake. Lakini Abdull hakuamini kwamba angerudi tena Mogadishu.
Baada ya dakika kadhaa waliagana lakini Fartuun hakuacha kusisitiza kwamba atamsubiri .
Alimwachia Abdull zawadi ya saa, aliamini huenda itakuwa kumbukumbu kubwa sana kwake, pengine moyo wake ungejirudi na kuamua kurudi Somalia siku moja, kupitia ile zawadi ambayo alimuachia.
Siku iliyofuata ndio safari ilipoanza, hata Abdull aliporudi nyumbani alimkuta Talib akiwa ameshakunja kila kitu, tayari tu kwa ajili ya kuondoka.
Kuliopokucha, walitumia usafiri wa ndege kutoka Mogadishu hadi Nairobi. Asubuhi ile Fartuun naye aliamka mapema na kukimbilia nyumbani kwao Abdull tena, akiwa na matumaini atamuona kwa mara ya mwisho, pia alikuwa na zawadi nyegine kwa ajili yake, lakini hakuwakuta tena walikuwa wameshaondoka mapema mno.
Walipofika Nairobi walikaa siku moja katika hoteli, hali ya hewa ilikuwa ni baridi sana, baada ya siku kupita walipanda tena ndege kutoka Nairobi hadi Arusha. Napo walikaa siku moja tu , hawakupendelea kubaki sana katika miji hii kwa sababu ya baridi iliyokuwa inapepea kwa wakati sana.

Baada ya hapo safari ikawa ni kuelekea katika mji wa Dodoma, walipofika kwa basi walikaa katika hoteli kwa muda wa wiki nzima. Wakitembea katika mji wa Dodoma nyakati za jioni pevu. Abdull hakuhitajika kuonekana sana kwa sababu ya kile kilichomleta katika mji huo.
“Hukunieleza, kwanini ulimuacha mke wako?, Abdull alimuuliza Talib wakiwa wanatembea katika soko moja Dodoma mjini, yalikuwa ni majira ya saa kumi na mbili jioni.
“Hata na wewe hukunieleza kuhusu yule binti..”
Baada ya Talib kuulizwa na yeye kuuliza, ilibidi wote wanyamaze na kuziwacha mada hizo kwani kila mmoja hakuonekana kuwa tayari kumueleza mwenzake, juu ya masuala yale.
Siku ile ilikuwa ni ya mwisho kwa Abdull kuishi uraiani. Baada ya kumaliza chakula chao cha mwisho wa siku, walichokipata katika baa moja jirani na soko, waliamua kurejea katika chumba chao cha hoteli.
Asubuhi kulipokucha, walichukua usafiri wa Taxi na kuelekea katika Hospitali ya Afya ya Akili Mirembe. Awali Talib alishamsisitiza Abdull kwamba ataingia pale kama mgonjwa wa akili, mpango mzima wa mauaji waliyoyakusudia ilibidi uanzie Mirembe.
Lakini Mirembe hawakuingia kwa ajili ya kuuwa, isipokuwa ni kufanikisha katika moja ya njia ya kufanikisha safari yao nzima ya mauaji ya rais , kama mpango unavyoelekeza.
Halikuwa jambo gumu kukubaliwa hospitali pale kwa sababu, Abdull alionekana kiudhati kwamba ni mgonjwa wa akili, alibadilika na kuwa hivyo tangu wanatoka katika hoteli. Lakini wao wawili tu ndio walielewa kwanini wameamua kufanya vile.
Abdull alibaki hospitali pale, na kuanza kuhudumiwa kama wagonjwa wengine. Talib akaondoka na kufunga safari ya kurudi Somalia baada ya siku chache, lengo ni kuenda kuzishughulikia biashara zao ambazo wameziacha.
Somalia mambo yaliendelea kuwa mazuri,ingawa mabomu ya mapambano yalikuwa yanatokea mara kwa mara, lakini bado mji wa Mogadishu ulikuwa chini ya serekali ya Somalia.
Kila baada ya miezi miwili Talib alikuwa anakwenda Dodoma kumjuulia hali mdogo wake, kuna wakati akisitishwa na hali ya mdogo wake katika hospitali ile kwani mwili wake ulipungua kidogo. Abdull aliamua kuishi maisha ya uchizi kwa asilimia zote ili asije kugundulika.
Wote wliamini ndio njia sahihi walioamua kuichagua wote wawili ili kukamilisha walilopanga na kuikata kiu yao ya kisasi.
Abdull akikutana na madaktari mara kwa mara ili kupata msaada wa kurudisha akili yake sawa, hawakuwa wanaelewa kwamba haukuwa uchizi wa ukweli lakini ni wa kuigiza .
Miezi ilikatika , hadi mwaka na hatimaye alitambulika rasmi kwamba ni mgonjwa wa akili, akapatiwa na cheti cha kutambuliwa kutoka katika hospitali ile ya serekalini, kwamba ana matatizo ya akili.
Wiki moja kabla ya Talib kurudi Dodoma kwa ajili ya kwenda kumtoa Abdull ili wasonge mbele katika mpango wao. Jioni moja akiwa amejipumzisha katika bustani ya nyumba yake katika mji wa Mogadishu, alitembelewa na Fartuun.
Mwaka ulikuwa umeshakatika, Fartuun alikuwa ni muajiriwa wa benki moja katika mji wa Mogadishu. Alikuwa amenawiri ukimuangalia, mwili wake haukuonekana kuwa na njaa ya kimaisha lakini uso wake uliashiria bado moyoni ana njaa na mtu fulani.
“Nakuona wewe tu, Abdull yuko wap?, alimuuliza baada ya samalamu na makaribisho.
Talib aliinua kichwa chake na kumtazama usoni, aliona uso wa hamu aliokuwa nao Fartuun kutaka kujua Abdull yuko wapi. Lakini swali hili la sasa lilishaanza kuwa na dalili ya ugumu juu ya jawabu yake.
“Nambie yuko wapi, simu yake siipati tena…”, Talib alibaki tu akimuangalia bila ya hata jibu, alibaki anazungusha kichwa chake huku na kule.
“Umeshaolewa?
“Jibu swali langu kwanza” kisha akachukua glasi ya maji kuzimua koo lake.
Baada ya mabishano ya hapa na pale, hatimaye Talib alimuomba Fartuun amsubiri hadi atakaporudi tena Tanzania, ndipo atakuja na jawabu sahihi juu ya swali lake.
Fartuun alielewa ni muendelezo tu kuzungushwa bila ya kuelezwa Abdull yuko wapi, kwani kichwani mwake alijua wazi kwamba hakushindwa kujua alipo wakati waliondoka wote.
Lakini hakutaka kuendelea kusisitiza aelezwe alipo , hasa akikumbuka kwamba Abdull mwenyewe hakutaka kuweka wazi anaenda Tanzania sehemu gani na kwa kazi ipi hasa.
“Nimezoeya nimesubiri mwaka nzima ..sishindwi kusubiri mwaka mwengine..”
Baada ya wiki kumiliza Talib alirudi Morogoro na kwenda kufanya taratibu za kumtoa hospital Abdull.
Baada ya kufanikisha taratibu zote, ndipo walipoondoka Dodoma baada ya mapumziko ya siku chache na kuanza safari ya kuelekea Dar es Salaam, kisha wakafika Zanzibar ambako ndiko tukio la mauji lingefanyika.
*********************
Siku, wiki na na miezi tisa ilikatika tangu Abdull na kaka yake waanze maisha yao Mji Mkongwe, kila mtu alijua Abdull ana tatizo la akili, alikuwa mzururaji mkubwa katika vichochoro na mitaa.
“Abdull ondoka juani basi?, ilikuwa ni sauti ya Najma , alipomkuta kalala kwenye kibaraza kimoja jua likimpiga. Bila ya kuchelewa Abdull aliinuka na kwenda upande mwengine.
Familia ya Najma ni marafiki wakubwa sana wa Abdull, tangu siku Baba yake Najma , ambaye ni Issa alipomkuta kalala pembezoni mwa nyumba yao akiwa na njaa kali, akaamua kumsaidia kwa maji na chakula.
Baba wa Najma kwa jina la maarufu Sheikh Issa ni mzee wa takribani miaka sabini na kitu, Najma ni mtoto wao pekee. Katika nyumba yao, anaishi yeye na wazazi wake pamoja na mfanyakazi wao wa kike.
Licha ya tatizo la akili wanaloamini Abdull analo, bado waliendelea kuwa karibu naye wa sababu ya upole na utulivu aliona nao. Sheikh Issa aliutumia muda wake mwingi katika duka lake la vyakula, ambalo limeungana na nyumba yake.
Najma ni binti wa miaka 26,alimaliza shahada yake ya masuala ya biashara katika chuo Kikuu kimoja kilichopo katika jiji la Dar es Salaam, takriban mwaka na nusu uliopita.
Alipata kazi lakini kwa bahati mbaya aliachishwa kazi hiyo , katika kampuni moja ya kibiashara, baada ya kampuni kufilisika.
Baada ya kusimamishwa kazi na wafanyakazi wengine wengi, akaamua kutumia muda wake mwingi kumsaidia Baba yake katika shughuli za dukani, huku akiendelea kutafuta kazi nyengine.
Mchana ule Najma alipomkuta Abdull juani, alikua anaelekea sokoni kwenda kutafuta kitoweo, shughuli nyingi za nje ya nyumba alikuwa anazifanya yeye au mfanyakazi wao.
Talib aliendelea kuishi pamoja na Abdull lakini mara kwa mara huondoka na kurudi Somali kwenda kuhakikisha biashara yao inaenda sawa. Rafiki yao mmoja kwa jina la Iddrisa, ndiye walimkabidhi kusimamia kwa kipindi ambacho wao hawapo.
Jua lilipozama na kiza kufunika kila kona, Abdull alikuwa tayari amesharudi nyumbani kwao Vuga.
“Hutoamini, naend Somalia lakini sijabahatika kuonana na Fartuun tena mwaka unakaribia..”, Talib alisema wakati wakipata chakula cha usiku.
“Ukienda tena mtafut, mfate kwao..”
Baada ya mazungumzo marefu hatimaye wote wakaingia kitandani kulala, wakiamini zile siku za kutekeleza kile kilichowaleta Zanzibar tayari zimeanza kukaribia.
Kama kawaida jua likichomoza Abdull huamka na kuanza kuzurura katika mitaa ya mji Mkongwe, maskani yake kubwa ni eneo la Mkunazini katika duka na nyumba ya Sheikh Issa.
Asubuhi ya siku ile alimkuta Najma dukani, kama kawaida ya Najma hupenda kumpumbaza Abdull.
Alimuuliza , ikitokea kuna wanaume wawili wanamtaka ili wamuoe, mmoja akiwa na pesa sana lakini mwengine hana pesa, na huyo asiye na pesa ndio anampenda pia.
“Abdull unadhani kwangu bora ni yupi?,” alisukuma pumbazo lake kisha akawa anatabasamu kusubiri jawabu kutoka kwa mgonjwa wa akili.
“Usiwe na tatizo la kutafuta fakhari ya macho, furaha ya moyo ndilo jambo muhimu..”, alijibu kwa sauti ya chini kama ananong’oneza.
“Sijakuelewa” alidakia, kisha akakaa vizuri kumsikiliza
“Furaha ya moyo ni kuwa na mtu unayempenda… katika maisha furaha ya moyo ndio jambo muhimu”, alimaliza akainuka na kuodoka.
Najma alibaki akimpigia mayowe ili arudi lakini alikatisha chochoro na kutokomea katika mitaa mengine, akimuacha Najma akishangaa na kubaki mdomo wazo kwa sababu ya uzuri wa jawabu yake.
Kupenda huku kumpumbaza Abdull kumbe ana lake moyoni, ameshauoana uwezo mzuri wa Abdull katika kufirikia na kutoa mawazo katika mambo tofauti.
Haikuwa siku ya kwanza Najma kupewa jawabu zuri miongoni mwa maswali anayomuuliza Abdull. Alishawahi hata kumwambia Mam
a yake kwamba anahisi Abdull ana uwezo wa kuzungumza mambo ya msingi wakati mwengine.
Analikumbuka tukio la kwanza kuliona lililomfanya kushagazwa na uwezo wake ni pale, alipomkuta anazunguza Kiengereza safi na baadhi ya watalii waliokuwa wakipita.
Kutoka hapo alijitahidi kumkera kera ili amwambie kiwango cha elimu yake, au amejuaje kuzungumza kiengereza kizuri lakini ni swali ambalo daima Abdull hukwepa kujibu.
Nini kitafuata sehemu ijayo? Najma atakuwa na mchango wowote katika tukio linaloenda kutendeka? Vip kuhusu Fartuun na familia yake bado anaendelea kumsubiri Abdull au ameshaingia katika maisha mengine? Tukutane wiki ijayo…