Taasisi ya Twaweza imebaini asilimia 60 ya wananchi hawajisikii huru kukosoa Taasisi ya Rais huku asilimia 54 hawajisikii huru kumkosa Makamu wa raisi.
Utafiti huo uliotumwa leo Machi 29 kwa vyombo vya habari, umeeleza kuwa idadi kubwa ya wananchi wamesema wanapaswa kuwa huru kuikosoa serekali na Taasisi ya Rais inapofanya uamuzi mbaya.
Pia utafiti huo umebainisha kuwa asilimia 71 ya wananchi hawaungi mkono matumizi ya lugha za matusi, wametaka Watanzania wasiruhisiwe kuwaita wafuasi wa chama chochote cha siasa “wapumbavu au malofa”.
Takwimu za muhtasari wa utafiti huo kwa jina la “Siyo kwa kiasi hicho? Maoni ya Wananchi kuhusu Taarifa na Mijadala”, uliofanyika Tanzania Bara na Zanzibar, umewahoji wananchi 1,519 kutoka awamu ya 25 ya kundi la pili la Sauti za Wananchi, zilizokusanywa kati ya Novemba 7 na Novemba 27, 2017.