Katika kile kinachoibua hisia za Maalim Seif Sharif Hamad kwa kusalitiwa na baadhi ya jamaa zake wa Pemba kwenye mgogoro wa chama chake unaoendelea sasa, Katibu Mkuu huyo wa Chama cha Wananchi (CUF) ametoa kauli kali zaidi kuwahi kutolewa naye hadharani dhidi ya kundi la wanasiasa hao waliomgeuka, hasa Khalifa Suleiman Khalifa, aliyewahi kuwa mbunge wa muda mrefu wa jimbo la Gando, Wilaya ya Wete, kisiwani Pemba.