Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA), amewaonya vikali na waziwazi Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba; Mkuu wa Usalama wa Taifa, Modestus Kipilimba; na Mkuu wa Polisi Simon Sirro dhidi ya kile anachosema ni muelekeo wao wa kuipeleka Tanzania kwenye machafuko makubwa ya wenyewe kwa wenyewe.