Khofu mpya zimezuka baada ya Rais Donald Trump wa Marekani kuonya kuwa “Urusi haitoridhishwa” na jaribio la makombora ya masafa marefu lililofanywa hivi karibuni kabisa na Korea Kaskazini.
Utawala wa nchi hiyo ulifanya jaribio jengine tena kutokea pwani ya magharibi siku ya Jumamosi (Mei 14), na rais huyo wa Marekani alijibu kwa kuonesha namna kombora lilivyoangukia karibu sana na mpaka wa Urusi.
“Kwa kombora hili ambalo linaiathiri zaidi Urusi kuliko hata Japan, Rais Trump hafikirii ikiwa Urusi imeridhika,” ilisema taarifa ya Ikulu ya Marekani, White House.
Kombora hilo lilipaa umbali wa kilomita 700 na kufikia masafa ya zaidi ya kilomita 2,000, kwa mujibu wa maafisa wa Japan na Korea Kusini, hicho kikiwa kiwango cha juu zaidi kuliko makombora ya masafa ya kati yaliyojaribiwa na Korea Kaskazini mnamo mwezi Februari kutoka mkoa huo huo wa Kusong ulio kaskazini magharibi mwa mji mkuu, Pyongyang.
Filed under: HABARI Tagged: Korea Kaskazini, Marekani, Urusi
