Katika ziara yangu nchini Oman mnamo mwezi Machi, nilikutana na mashujaa wengi wa Zanzibar, ambao Zanzibar ya leo na Oman yenyewe pia haziwezi kusimama kujisemea zisiwasemee kama kweli zinataka kuweka rikodi yake sawa. Mmoja wao ni huyu Bibi Suad Al Lamki, ambaye alikuwa jaji wa pili tu mwanamke kwenye Mahakama ya Tanzania baada ya uhuru. Mazungumzo yangu naye, ambayo yapo hapo kwenye vidio, yanaibua mengi ambayo yumkini yalikuwa hayasemwi kuhusu Zanzibar ya kabla ya Mapinduzi na hata ya baadaye, nafasi ya ilimu na mwanamke kwenye jamii za Kiarabu na Kiislamu, na pia dhima ya taaluma kwenye maisha ya kifamilia.
Filed under: Kalamu ya Ghassani Tagged: kanuni, Oman, sharia, suad al lamki, Tanzania, Zanzibar
