WAKATI Mapinduzi yanafanyika tarehe 12 Januari 1964, baba yangu (Mungu amrehemu) alikuwa ndio kwanza amewasili kisiwani Unguja akitokea Bara, ambako alikuwa ameishi kwa takribani miaka mitano mtawalia. Katika pirikapirika za Mapinduzi hayo zilizoanza usiku wa Jumamosi, akakamatwa siku ya tatu yake na watu wenye silaha kutokea Bara akiwa mitaa ya Kikwajuni. Jambo la kwanza aliloulizwa … Continue reading Sisi ni kizazi cha waliopindua na waliopinduliwa
