Mimi ni zao la Zanzibar. Ni matokeo ya maelfu ya pepo za msimu zilizowapeperusha watu wa madau kutoka duniani kote kuja kwenye visiwa hivi viduchu vilivyochipuka katika maji vuguvugu ya Bahari ya Hindi mashariki mwa bara la Afrika. Wakati wafanyabiashara wa Bahari ya Hindi wakisambaza bidhaa zao, lugha ya Kiswahili ikaibuka sambamba na Waswahili pamoja na utamaduni wao. Ninaona fahari kuitwa Mswahili. Mimi ni mchanganyiko …
↧