Tangu Aprili 2015 alipolazimisha kuteuliwa na chama chake cha CNDD-FDD kuwania urais na kushinda uchaguzi huo uliofanyika Julai, zaidi ya watu 400 wamekufa katika mapambano kati ya vikosi vya serikali na raia wanaopinga rais huyo anayedaiwa mlokole kuongoza tena. Bila shaka Rais Ali Mohamed Shein ana jambo la kujifunza ili asiifikishe Zanzibar huko iliko Burundi. Historia ni mwalimu mzuri. Migogoro mingi ya kisiasa hutokana na …
↧