Ni bahati mbaya sana kwamba wengine wanauchukulia uungwana na ustaarabu wetu kwamba labda ni dalili ya udhaifu na wanadhani labda wanaweza kutuburuza. Kwa hilo, nawaambia wazi kwamba WASAHAU. Nataka niwahakikishie kwamba sisi si dhaifu ila tunaongozwa na uzalendo na mapenzi kwa nchi yetu na wananchi wenzetu. Lakini uzalendo huo huo na mapenzi hayo hayo kwa nchi yetu na wananchi wenzetu yanatutaka tusimame kuitetea na kuilinda …
↧