NILITULIA kumsikiliza Bernard Kamilius Membe akitangaza nia ya kuusaka urais wa Tanzania. Ilikuwa na maana kubwa kwangu kwa sababu kada huyu mwenye nguvu na kachero aliyejijenga nyumbani na ughaibuni, amesimama kama tishio kwa wengine wote. Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, ni mbunge wa Mtama, mkoani Lindi, kule kulikojaaliwa raslimali ya kiuchumi ya gesi. Nina rafiki zangu serikalini kama nilivyonao kwenye Chama Cha Mapinduzi (CCM). Wengi…
↧