Kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbali mbali watu saba wamethibitika kufa kutokana na mafuriko katika wilaya tatu za jiji la Dar es Salaam
Kamanda wa Kanda Maalumu ya Polisi Dar es salaam, Lazaro Mambosasa amethibitisha taarifa hizo ambapo amesema kuwa watu sita wameripotiwa kufariki katika wilaya za Kinondoni na Ilala huku mmoja akiripotiwa kufariki katika wilaya ya Temeke.
“Mpaka sasa tumepokea taarifa za vifo vya watu saba katika maeneno mbalimbali ya jiji la Dar es salaam ambapo watatu wamefariki wilaya ya Kinondoni, wengine watatu wilaya ya Ilala na mmoja umekutwa ukielea katika bonde la mto msimbazi. Hii ni kutokana na mvua kali zinazoendelea kunyesha jijini Dar es saalamu,“amesema kamanda Mambosasa.