Aliyekuwa mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba, amesema kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya chama hicho, Julius Mtatiro, hana heshima na hana adabu, akidai kuwa ni kijana aliyemleta mwenyewe kwenye chama na sasa amegeuka kuwa mshambuliaji mkubwa dhidi yake.