Mwenyekiti wa zamani wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amemlaumu Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad, kwa kupitishwa sheria ‘mbaya’ za uchaguzi kwenye Baraza la Wawakilishi la Zanzibar lenye wana-CCM watupu kwa madai kuwa kunatokana na katibu mkuu huyo kuzuwia kesi za wawakilishi wa CUF baada ya uchaguzi wa Oktoba 2015.