Chama cha Wananchi (CUF) kimelaani vikali hatua ya serikali ya Rais John Magufuli kulifungia gazeti huru la Mawiyo kwa kisingizio cha kuwahusisha marais wastaafu na kashfa ya mikataba ya ovyo kwenye sekta ya madini, ambayo imeitikisa nchi.
Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho upande wa Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui, ameiambia Zaima Media kwamba amri ya kukataza kujadiliwa dhima na mchango wa viongozi waliostaafu kwenye kuingia mikataba hiyo ni kinyume na katiba, demokrasia na utawala wa sheria na hata mantiki ya uongozi bora.
Angalia vidio yake hapo chini:
Filed under: VIDIO Tagged: cuf, demokrasia, haki, Mawiyo, Mazrui, Tanzania, uhuru wa habari
