Siku moja tu baada ya Rais John Magufuli kuonya vyombo vya habari dhidi ya kuwahusisha marais wastaafu na kashfa ya mikataba ya madini, waziri wake wa habari, Harrison Mwakyembe, amelifungia gazeti huru la Mawio kwa kipindi cha miaka miwili kuanzia leo kwa tuhuma za kuvunja amri hiyo.
Taarifa iliyotolewa na kusainiwa na mkuu wa Idara ya Habari na Maelezo ya Tanzania Bara, Hassan Abbas, inasema Waziri Mwakyembe amechukuwa hatua hiyo baada ya gazeti hilo kuchapisha picha za marais wastaafu, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete, kwenye habari inayohusu kashfa ya makinikia.
Adhabu hiyo ya miezi 24 inaanza kutekelezwa leo, ambapo Mawio imezuiwa kuchapishwa na kusambazwa hata mitandaoni.
Filed under: HABARI Tagged: Makinikia, Mawio
