Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, amesema serikali ya Zanzibar inayoongozwa sasa na Dk. Ali Mohamed Shein haipo kikatiba na kwamba lazima itaondoka.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mara tu baada ya kufungua ofisi za wabunge wa Chama chake, Maalim Seif alisema kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar, lazima serikali ya nchi hiyo iwe ya umoja wa kitaifa na pia iwe imetokana na uchaguzi halali, sifa zote mbili zinakosekana kwenye serikali ya Dk. Shein.
Filed under: VIDIO Tagged: CCM, cuf, maalim seif, shein, Zanzibar
