Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, jana alimkaribisha na baadaye kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Taasisi ya Kimarekani inayoshughulikia masuala ya Demokrasia Duniani (NDI), Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Dr. Keith Jennings, na ujumbe wake katika Makao Makuu ya CUF, Mtendeni mjini Zanzibar, leo.
Wengine walioshiriki mazungumzo hayo kutoka Taasisi hiyo ya NDI ni Mkurugenzi Mkaazi (Tanzania), Bibi Sandy Quimbaya, Mkurugenzi Mkaazi anayemaliza muda wake, Bodunrin Adebo, na Afisa Mipango wa NDI nchini Tanzania, Mahija Dodd.
Kwa upande wa CUF, mbali ya Maalim Seif, mazungumzo hayo yaliwashirikisha pia Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa wa CUF, Ismail Jussa, na Katibu wa Maalim Seif, Issa Kheir Hussein.
Filed under: HABARI
