Wabunge wa Chama cha Wananchi (CUF) wamewatuhumu moja kwa moja waziri na naibu waziri wa mambo ya ndani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kile walichosema ni ushiriki wa moja kwa moja wa viongozi hao kwenye kuupandikiza na kuuchochea mgogoro wa kiuongozi unaokikumba chama hicho.
Mbunge wa Tandahimba, Katani Katani, na Khatib Said wa Konde, walitumia muda wao wa dakika tano tano kuchangia hotuba ya bajeti ya wizara ya mambo ya ndani leo kuanika “ushiriki wa wizara” hiyo kwa ujumla wake na ule wa Naibu Waziri Masauni kwa upande wake kwenye matukio mbali mbali ambayo katika ujumla wake wameyaita ni hujuma za wanasiasa hao dhidi ya CUF. Sikiliza sauti zao hapo chini:
https://m.soundcloud.com/mohammed-k-ghassani/mbunge-wa-tandahimba-ampa
https://m.soundcloud.com/mohammed-k-ghassani/tuliyavumilia-ya-lipumba-ili
Filed under: SAUTI
