Wakati Rais wa Tatu wa Zanzibar na wa Pili wa Tanzania, Mzee Ali Hassan Mwinyi, maarufu kama Mzee Ruksa, akiadhimisha umri wa miaka 92 tangu azaliwe, huenda moja ya zawadi alizopatiwa na Mzanzibari huyu ikawa ndiyo bora zaidi kuwahi kupokea maishani mwake mote.
Soma hapa waraka wa Said Miraaj, mwanasiasa wa siku nyingi visiwani Zanzibar akimtakia kheri ya kuzaliwa Mzee Mwinyi.
TAFAKURI YA BABU.
HONGERA KWA KUTIMIZA MIAKA 92 YA KUZALIWA SHEIKH ALI HASSAN MWINYI.
Leo ni siku ya kumbu kumbu ya kuzaliwa kwa aliekuwa rais wa pili wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania, Sheikh Ali Hassan Mwinyi.
Kwa kawaida vijana wa kisasa siku kama ya leo hufanya sherehe na kukata keki huku wakinywa vinywaji ili kuonyesha furaha yao. Lakini kwa wazee kama sisi aghlabu pamoja na maambo mengine huitumia siku kama ya leo kumshukuru mungu kwa kutufikisha umri tulio nao, kutafakari masiku yetu yaliyopita, kujipanga kwa masiku yajao ili tuweze kujikurubisha kwa Mungu zadi, hua tunaomba msamaha na kufanya toba kusudi kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu na kuomba Khusunul”khatima tuu, yaani mwisho mwema katika dunia.
Leo natumia fursa hii kumuasa na kumuomba kwa nasaha Mzee wangu Sheikh Ali Hassan Mwinyi, yafuatayo:-
Kwanza Shekhe Ali Hassan Mwinyi, nakuomba umshukuru Mwenyezi Mungu kwa kukujaalia umri huu wa zaidi ya miaka tisiini kwa zama hizi na kua bado una afya nzuri na ukali jiweza, haya ni mapenzi makubwa toka kwa mola wako, kesha ukimshukuru.
Pili mshukuru Allah kwa neema alizo kukirimu ikiwemo, afya, elimu, utukufu, uluwa, umaarufu, kiasi cha mali si haba, maisha yenye wastwaa japo si makubwa kama wengine, watoto wenye mafanikinko ya kimaisha nk.
Tatu karama ya kupendwa na uliowaongoza kwa muda wote ulipokua madarakani. Shekhe Ali ni wewe tuu Mwenyezi Mungu aliekupa fursa ya kuwa Rais wa Zanzibar na kisha ukawa pia Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, neema hii hayupo àliepewa tena hadi sasa katika nchi hii zaidi yako.
Wewe Sheikh Ali ndie kiongozi pekee uliepigiwa kura na kupata asilimia kubwa ya kuungwa mkono katika visiwa vya Zanzibar tokea uhuru na hayupo aliekufikia.
Shekhe Ali ni wewe tuu ulie zaa mtoto ambae kisiasa hadi sasa amewahi kuwa Mbunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano kwa majimbo mawili moja likiwa la Kwahani Zanzibar na jengine likiwa la Mkuranga katika mkoa wa pwani huku Mrima.
Hakika tukitaka kuhesabu neema ulizokirimiwa na Mola hatuwezi kuzimaliza.
Ila.pamoja na neema hizo zote ni wewe tuu ambae Mwenyezi Mungu aliye kupa majaribu kwa jambo ambalo halijawahi kutokea kwa kiongozi yeyote wa kaliba yako katika nchi hii tokea uhuru hadi sasa.
Shekhe Ali yakupasa utafakari sana ni kwa nini Mungu alikuonja kwa mtihani huu pamoja na neema alizokukirimu za kulindwa na kadhalika tena mbele ya kadamnasi?
Tulisoma katika kitabu kitakatifu kwamba hakika ya kila jambo huwa na sababu yake “In’na sabab’naa limaa’aswab’ba” ni imani iliyojengeka kwamba hadi ukaonekana kuwa unafaa kuiongoza jamuhuri baada ya kuondoka Mwalimu kwamba sababu yake ulionekana na kupendeza ulipokua rais wa Zanzibar, yumkin ulifanya vizuri kulikoni ilivyo tazamiwa.
Alaakulihali ni kwamba Shekh Ali uliwaacha Wazanzibari wakati bado wakikuhitaji, uliwaacha wanyonge hawa walio kupa mapenzi makubwa, utiifu sambamba na uaminifu kwako wakiwa wanahitaji kuunganishwa ili wasahau mifarakano ya masiku yaliyopita, vizazi vilihitaji kutolewa katika wimbi la ukabila na uzawa ambapo wakati wa uongozi wako hakukuwepo na mitazamo ya rangi, kabila, wala mahali mtu alipotoka, wazanzibari walikupa fursa ambayo hajawahi kupewa kiongozi yeyote katika Zanzibar kutoka CCM.
Leo Sheikh Ali Hassan Mwinyi una miaka 92, unadhani wazanzibari wakukumbuke kwa lipi siku Mola wako atakapo kuhitaji zaidi ya kuonyesha shukurani kwa kusaidia kuwarejeshea umoja ambao ulikoma ulipoondoka?
Wanao jitahidi wanajitahidi tatizo ni kuaminiana wewe wazanzibari walikuamini na sifa ya muungwana akiaminiwa huwa hakhini.
Sheikh Ali leo umekua Shaib (Mzee), najua umuumini tena unàejitahidi katika kutafuta njia sahihi ya kufata, jee huoni kua njia hii ndio malipo pekee kwa wema wakiokufanyia wazanzibari na itawafanya wazanzibari wakukumbuke zaidi kwa wema wako siku ukitika wito wa muumba wetu?
TAFAKARI.
Filed under: JAMII Tagged: Ali Hassan Mwinyi, birthday, sherehe ya kuzaliwa, Tanzania, Zanzibar
