Huenda Emmanuel Macron ndiye rais kijana zaidi kuliko wote waliowahi kuitawala Ufaransa, lakini pia huenda mkewe akawa mkongwe zaidi kwa mwanamme huyo mwenye umri wa miaka 39 kuliko wake wengi wa maraisi Ulaya ya Magharibi.
Uhusiano kati ya wawili hawa umeutikisa ulimwengu, ingawa yumkini hakuna kitu kikubwa sana kwenye hadithi yao ya mapenzi iliyoanza wakati Macron akiwa mvulana wa miaka 15 tu akisoma skuli ambayo ikiongozwa na Brigitte Trogneux aliyekuwa mkubwa wake kwa miaka 24.
Punde, Brigitte akabadilika kutoka kuwa mwalimu wa Emmanuel hadi kuwa mwenza wa kimapenzi na baadaye mkewe. Lakini katika kila hatua, aliendelea na kubakia kuwa shujaa na kichocheo cha mabadiliko kwa mumewe huyu.
“Bila ya Brigitte, nisingelikuwa mimi!” Alitangaza hadharani Macron jana wakati akiupokea ushindi wa asilimia 65 za kura kuwa rais mpya wa Jamhuri ya Ufaransa.
Hivi sasa Brigitte ana wajukuu saba na umri wa miaka 64 na Macron ana miaka 39 na hana mtoto wa kumzaa, lakini hadithi yao ya mapenzi na familia haina ukomo.
Tangu kwenye kampeni zake, Macron alishasema wazi kuwa sio tu Brigitte atakuwa mke wa rais, bali pia atakuwa na nafasi rasmi kwenye serikali yake.
Filed under: BURUDANI Tagged: Brigitte, Emmanuel Macron, Ufaransa
