Si kawaida mafuriko kukiathiri kisiwa cha Pemba, hata panapokuwa na mvua kubwa kiasi gani, kutokana na maumbile yake ya milima na mabonde, lakini mvua kubwa ya masika inayoendelea sasa imezamisha madaraja kadhaa, kuporomosha milima, kuvunja majumba na kugharakisha mashamba.
Click to view slideshow.Hadi sasa, hakujakuwa na taarifa za vifo au watu waliopotea lakini hali ni mbaya sana. Ripoti kutoka huko zinasema familia zaidi ya 200 katika mkoa wa Kusini zimepoteza makaazi, mashamba na mali zao. Msaada mkubwa wa kibinaadamu unahitajika haraka. Msikilize mzee huyu akiisimulia hali kama anavyoishuhudia kwa macho yake.
Filed under: HABARI Tagged: gharika, mvua, pemba, Zanzibar
