Tokea Chama cha Mapinduzi (CCM) kupata kipigo cha kihistoria katika Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar wa tarehe 25 Oktoba, 2015 ambapo kilizidiwa na Chama cha Wananchi (CUF) kwa kura 25,831 kimekuwa kikiweweseka kwa madai ya kwamba kimeibiwa kura kisiwani Pemba na hivyo kutoa mashindikizo kwamba matokeo ya uchaguzi huo yafutwe. Sisi CUF tulikuwa tukiwaeleza ukweli tokea wakati wa kampeni kwamba kuzidiwa kwa CCM katika oganaizesheni na …
↧