UCHAGUZI mkuu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na uchaguzi wa kumchagua Rais wa Zanzibar unaotarajiwa Oktoba 25 unakabiliwa na mtihani mgumu kutokana na kampeni chafu inayoendeshwa na makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Ni Dk. Ali Mohamed Shein peke yake anayeeleza atawafanyia nini wananchi akichaguliwa tena akianzia na kutaja mafanikio ya serikali tangu 2010, na kutoa ahadi mpya nyingi na kubwa zisizotekelezeka. …
↧