Al Bashir hakuwa na uungwana huo. Aliipindua serikali iliyochaguliwa ya Waziri Mkuu Sadiq al Mahdi baada ya serikali hiyo kuanza mashauriano na waasi wa Sudan Kusini. Ajabu ya mambo ni kwamba miaka kadhaa baadaye mnamo 2005, al Bashir alifanikiwa kuvikomesha vita vya pili vya wenyewe kwa wenyewe na kuwezesha pafanywe kura ya maoni ambayo hatimaye iliigawa sehemu ya kusini iwe taifa huru la Sudan Kusini.
↧