Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, amesema amefarijika sana kuona Kanisa la Kilutheri la Tanzania (KKKT) limetoa waraka wa kuzungumzia hali halisi ya nchi katika wakati ambapo vitendo vinavyokinzana na misingi ya taifa vikishamiri, akieleza kwamba si sahihi kuwakataza viongozi wa kidini kutoa maoni yao kuhusu mambo yanayoigusa moja kwa moja jamii yao, wakiwamo waumini wanaowafuata.