Licha ya juhudi kubwa za kuisaidia Tanzania kupitia miradi mbali mbali inayofadhiliwa kimataifa, mingi mingoni mwa miradi hio hufa muda mfupi baada ya kuanzishwa. Mwaka 2005, Benki ya Dunia ilitowa ufadhili wa mabilioni kadhaa kupitia ‘Mradi wa SP’, ambao ulikuwa makhsusi kwa uwekaji wa taa za barabarani kwenye mitaa na wilaya kadhaa jijini Dar es Salaam. Hata hivyo, taa hizo ziliwaka kwa wiki moja na baada ya hapo hakuna kilichoendelea tena, huku baadhi ya vifaa vikitoweka taratibu. Sasa wananchi wanalalamika.
ANGALIA VIDIO: Watoto wenye ulemavu wapatiwa njia za kisasa kujifunza