Wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA Secondary) wameibuka tena na ushindi kwenye jukwaa la kimataifa, baada ya kushinda tuzo ya biashara katika mashindano yafahamikayo kama ‘School Enterprise Challenge‘ yaliyozishirikisha nchi zaidi ya 100 ulimwenguni chini ya shirika la British Charity kupitia mradi wa Teach a Man to Fish.