Mbunge wa Ubungo kwa tiketi ya CHADEMA, Saeed Kubenea, amemtaka kwa mara nyengine tena Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba (CCM), kujiuzulu nafasi yake akimtuhumu kuwa hawezi tena kuaminika kushikilia wadhifa huo baada ya mkururo wa matukio ya mauaji na uvunjwaji wa haki za binaadamu unaofanywa na vyombo vilivyo chini yake, likiwemo tukio la kuuawa kwa mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji, Akwilina Akwilini.