Kamati ya manasheria mashuhuri wa Zanzibar ina dhumuni la kusimamia mpaka kufanikiwa kwa madai ya wazanzibari ya kurejeshewa:
• Mamlaka Kamili ya Zanzibar (Sovereign Zanzibar)
• Katiba Mpya ya kidemokresia halisi, Utawala Bora na Haki za Binadam
• Mipango ya maendeleo ya uchumi na ustawi wa Wazanzibari wote bila ya ubaguzi wa aina yoyote
Endapo mpaka mwisho wa mwezi wa Septemba 2017 Rais wa Zanzibar, Dokta Ali M. Shein na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hawakuitisha kura ya maoni chini wa uangalizi wa Umoja wa Mataifa itakayowauliza Wazanzibari endapo wanataka kuendelea na Muungano na Tanganyika au wanapendelea uhuru kamili wa Zanzibar.
Wazanzibari kupitia Kamati hii ya wanasheria mashuhuri wa Zanzibar watawasiliana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa aitake Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ichukue hatua muafaka na za haraka kuiwezesha Zanzibar kukikalia kiti chake cha Umoja wa Mataifa kabla ya December 2017 ili kuirejeshea Zanzibar uhuru wake uliopotea tangu Muungano wake na Tanganyika.
Endapo Tanzania itakataa kutekeleza haya itatubidi Wazanzibari tushauriane ili tupate matlaba yetu kupitia Umoja wa Mataifa New York. Wazanzibari inawabidi wachukue hatua za haraka za kisiasa kikatiba na kisheria ili kuirejeshea Zanzibar Mamlaka Kamili kitaifa na kimataifa ili kurekibisha hali halisi tangu kuundwa kwa Muungano wa Zanzibar na Tanganyika.
Wazanzibari wanasisitiza umuhimu wa amani na utulivu mpaka Zanzibar iwe tena taifa huru kwa kupitia njia na taratibu za sheria za kimataifa na katiba ya Umoja wa Mataifa.
Taarifa hii imetolewa na Balozi Salim Said Rashid, Katibu wa Kwanza wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar – 1964
Filed under: HABARI
