Leo ndiyo siku ambayo Rais John Magufuli anatazamiwa kupokea kile kiitwacho “Ripoti ya mchanga wa dhahabu”, huku bunge likiambiwa utalii umeongezeka maradufu ndani ya kipindi cha mwaka mmoja uliopita na mapato yake kuongezeka hadi trilioni 5, wakati ndugu wa Marehemu Salum Mohammed Bin Almasi aliyeuawa wiki mbili zilizopita na polisi kwa madai ya ujambazi wakiendelea kuususia mwili wa ndugu yao kwa mazishi na huko kwenye safu za michezo, Yussuf Manji aitosa Yanga.
Filed under: MAGAZETINI LEO Tagged: magazeti, Magufuli, Manji, Tanzania
