Mchana wa leo, Rais Muhamadu Buhari wa Nigeria amewakaribisha wasichana 82 walioachiliwa huru na kundi la wanamgambo wa Boko Haram, miaka mitatu baada ya kuwachukuwa mateka wakiwa kwenye skuli yao katika kijiji cha Chibok, jimbo la Borno.
Wasichana hao waliochiliwa kufuatia mazungumzo ya serikali ya Buhari na Boko Haram, ni sehemu tu ya wasichana 200 waliotekwa mwaka 2014.
Angalia picha za mkutano wa Buhari na wasichana hao 82 katika jengo la Aso Rock Villa hapo chini:
Click to view slideshow.Filed under: HABARI
