Nasikia mwasemani, mungalijinong’onea Nasikia kwa yakini, njama mnonipangia Nasikia tambueni, kama mwataka nibwia Mwanong’ona kitu gani, na yote nayasikia? Mbona yaja sikioni, si kushoto la kulia Sauti zingawa chini, kelele zinanijia Mwanong’ona ndani ndani, madili kunipangia Mwanong’ona kitu gani, na yote nayasikia? Naona muko shidani, mungalikinishikilia Mikono nitawapeni, pingu mupate nitia Sikio langu kichwani, hamuwezi lipatia Mwanong’ona kitu gani, na […]
↧