Ama itaniinuwa, au itaniangusha Na ama itaniuwa, au itanihuisha Lolote litalokuwa, sitaiwacha maisha Ama itanichukuwa, na mbali kunifikisha Au itanipinduwa, na nyuma kunirudisha Lakini havitakuwa, nayo kunitenganisha Lolote litalokuwa, ama itosababisha Ama kiwake kijuwa, au wingu likanyesha Tayari nishaamuwa, kwayo sitojiondosha Mohammed K. Ghassani 23 Februari 2016 BonnFiled under: Ushairi Tagged: maisha, Ushairi
↧