Kumeibuka kamatakamata ya watu wanaotuhumiwa kuhusika na miripuko ya mabomu katika maeneo mbalimbali ya Mji wa Zanzibar na baadaye wahusika husafirishwa nyakati za usiku kwenda Tanzania Bara, imefahamika visiwani humu jana. Madai hayo yametolewa na familia za watu hao wakati walipozungumza na waandishi wa habari Kikwajuni, Welesi mjini hapa na kudai kuwa watu kadhaa wameshakamatwa […]
